Ingia / Jisajili

Natamani Kujongea

Mtunzi: Fr. Aloyce Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Aloyce Msigwa

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 5,007 | Umetazamwa mara 10,555

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Natamani kujongea kwenye altare yako ili nami nishiriki kwenye karamu ya Bwana Yesu x2

Ni uone uzuri wa Bwana uliomo katika fumbo takatifu la Ekaristi mwili na damu ya Yesu

Nimpokee Bwana Yesu Kristu na kuishi pamoja nae siku zote akae ndani yangu nami ndani yake

1.       Bwana naomba unijalie moyo wa uchaji nitubu dhambi nami nijongee meza yako

Ninakuomba unijalie usafi wa moyo nikupokee nikiwa katika hali njema

2.       Karamu yako ni takatifu tena ya amani iliyojaa upendo na uzima milele

Na wale watakao shiriki kwenye meza imewapasa kujua vema siri yako

3.       Uwajalie huruma yako na mapendo yako uwatie nguvu wote wasio kupokea

Kwa nguvu yako uwainue walioanguka waondoe vizuizi vinavyo waangusha

4.       Uwaalike wanao wote kwenye meza yako waishiriki karamu ya uzima wa milele

Wafurahie amani yako na mapendo yako yaliyofichwa kwenye fumbo hili takatifu


Maoni - Toa Maoni

Mitao Renatus Jul 27, 2020
Wimbo mzuri mno hakika isipokuwa Mtunzi amekosewa mtunzi wake Anaitwa Athanas John Msangule(A.J.Msangule/Msangule A.J )Toka Ruanda Mbeya ambae pia ni mtunzi wa wimbo wa Nampenda Mungu wa 2 4 pia Watu hawatalingana 6 8 ambazo hizo nyimbo zote tatu zimerekodiwa unga ltd na kwaya ya moyo safi wa mama Bikira maria albamu ya baada ya Enyi watu wote pigeni makofi/Nikupe nini Ee Mungu

Regnald Mbughi Jul 31, 2019
Wimbo mzuri sana. Ila nadhani mtunzi ni mwalimu J. Msangule wa Ruanda Mbeya.

mary Jan 13, 2017
wimbo huu mzuri sana,na unatafakarisha mtu ajiulize na ajitakase kabla ya kuijongea meza

Toa Maoni yako hapa