Ingia / Jisajili

Uje Kwetu Roho Mtakatifu

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Pentekoste

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 234 | Umetazamwa mara 884

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Uje kwetu ewe Roho Mtakatifu - Uje ewe Roho Mtakatifu na Mfariji x2

1.Roho mwenye hekima Roho wa shauri na nguvu – Uje Roho

   Ewe mwanga wenye heri tujaze neema mioyoni – Uje Roho

2.U Mfariji mwema sana u rafiki wetu sote –

   Wape heri ya milele wanaokutumaini –

3.Roho mwenye uchaji washa moto wa mapendo –

   Bila nguvu yako Wewe binadamu hana kitu –

4.Ewe Roho wa Bwana kaa nasi tuelekeze –

   Wewe ni mfano mwema nasi sote tuuige –

5.Uwe nasi siku zote tupe heri ya milele –

   Tukutumikie Wewe leo kesho na milele –


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa