Ingia / Jisajili

Sifa Kwa Bwana

Mtunzi: Joachim Neander

Makundi Nyimbo: Kristu Mfalme | Shukrani

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 1,030 | Umetazamwa mara 2,696

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1. Sifa kwa Bwana Mwenyezi na mfalme muumbaji, Yeye ndiye afya nao ukombozi wa-ko. Jongeeni hekaluni mwa Bwana, njoni tumfanyie sha-ngwe

2. Mshukuruni na litukuzeni jina lake, kwani aleta faraja na neema tele. Usimshahau wala usimdharau anakupenda daima

3. Sifa kwa Bwana anayetawala dunia, anatulinda na kutuongoza daima. Uwinguni na duniani pote, Bwana ni mfalme mtawala

4. Msifuni Bwana Muumba mbingu na dunia, vionekanavyo na visivyoonekana. Bwana ni mkuu na jina lake pia, anastahili heshima

5. Malaika wanaimba sifa zake Bwana, na watakatifu hawachoki kumsifu. Nasi sote, tuungane pamoja kumshukuru Mwenyezi


Maoni - Toa Maoni

Kundaely Mar 29, 2020
Mnajitahidi kwa kuwafahamisha watu note za nyimbo mbalimbali

Toa Maoni yako hapa