Ingia / Jisajili

Ee Bwana Utuonyeshe Rehema Zako

Mtunzi: Himery Msigwa
> Mfahamu Zaidi Himery Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Himery Msigwa

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 856 | Umetazamwa mara 2,179

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 19 Mwaka A
- Katikati Dominika ya 15 Mwaka B

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Ee Bwana utuonyeshe rehema zako (Bwana) utupe rehema zako x 2

MASHAIRI.

1(A) Nanisikie atakavyosema Mungu Bwana maana atawaambia watu wake amani.

  (B) Hakika wokovu wake u karibu na wamchao utukufu ukae katika nchi yote.

2(A) Fadhili na kweli zimekutana haki na amani zimebusiana.

   (B) Kweli imechipuka katika nchi haki imechungulia kutoka mbinguni

3(A) Naam Bwana atatoa kilicho chema na nchi yetu itatoa mazao yake.

   (B) Haki itakwenda mbele zake nayoitazifanya hatua zake kuwa njia.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa