Ingia / Jisajili

Sasa Wakati Umefika

Mtunzi: Lukando Andrew Basil
> Tazama Nyimbo nyingine za Lukando Andrew Basil

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Philemon Kajomola

Umepakuliwa mara 5,540 | Umetazamwa mara 9,310

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Sasa wakati umefika wa kushika nilichonacho (mimi) 
Kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi 
Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu 
(Ili) Aone nilivyoandaa zawadi ya leo 
Nitamwambia Bwana pokea hiki kidogo nilichonacho 
Kwani Mungu wewe wanijua mimi siwezi hata kueleza 
Nakusihi sana Baba unipokee 
Nigawie na baraka niwe salama

 

 1. Mema yote niliyokuwa nayo yametoka kwa Mungu 
  Hivyo nami ni kosa kusahau kumshukuru 
  Kwani kuwepo hapa leo hii ni kazi ya nani 
  Kamwe mimi sitapata uwezo pasipo Mungu 
 2. Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi 
  Mbona hofu yazidi kuwa ndani ya moyo wangu 
  Mbele ya Bwana Mungu wangu kufanya siri ni bure 
  Yeye ndiye mpanga mambo yote ya wanadamu 
 3. Pumzi anayonipa uhai unatoka kwa nani 
  Bila Mungu hakika mwanadamu siwezi kitu 
  Nimepata nafasi hii leo ya kwenda kutoa zawadi 
  Heri niende ya kesho sio yangu ajua Mungu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa