Ingia / Jisajili

Nyimbo ninazopenda (My Favorite Songs)

Leo nimekuwa inspired na wimbo wa “Lukando Andrew Basil” unaoitwa “Tuimbe Bwana Amejifufua”. Nimeupenda wimbo huu, na ningependa sana kwaya yetu iimbe wimbo huu. Lakini, nilikumbana na changamoto moja. Wimbo huu ni wa Pasaka, na utahitajika mwakani kati ya mwezi wa pili mpaka wa nne (Inategemea pasaka itakuwa lini), je nifanyeje? Niliogopa nitaweza kuusahau wimbo huu.

 

Lakini pia, ni mara ngapi, unakutana na wimbo kwenye SMN ambao unaupenda sana, lakini huwezi kuu-print kwa wakati huo, na unaogopa unaweza ukausahau iwapo hauta – print wakati huo? Je utafanyeje?

 

Nikaona hitaji la kuongeza ‘functionality’ ya My Favorites. Kwa kifupi, wimbo wowote unaweza ukauweka kwenye “My Favorites” kwa kubofya kwenye link iliyoandikwa "Weka kwenye My Favorites" ambayo itakuwepo kwenye ukurasa wa wimbo huo. (Angalia picha hiyo).

 

 

Ukishabofya, wimbo huo utaongezwa kwenye favorites zako. – Kama hauko logged in, basi utalogin, kisha system itauongeza wimbo huo kwenye favorites zako.

 

Kwa ajili ya kuangalia nyimbo ambazo zipo kwenye favorites yako, yakupasa kwanza ulogin, kisha bofya link kama inavyoonekana hapo kwenye picha ili uone favorites zako. Enjoy.