Ingia / Jisajili

Je, nyimbo zako haziwi reviewed?

Kama wewe ni mmoja wa watu wanao-upload nyimbo mara kwa mara, basi walau mara moja au mbili au zaidi, umeona Admin haku-review nyimbo zako.

Kuna sababu mbili kuu za kutoreview:
 

 • Wimbo umo tayari kwenye Swahili Music Notes.
 • Wimbo haujafikia kiwango cha ubora kuwa kwenye site.

Sababu ya kwanza inajieleza wazi kabisa ila nadhani sababu ya pili ndo inahitaji maelezo zaidi.

Ninaposema kiwango cha ubora, simaanishi ubora wa kimuziki wa nyimbo. Mimi sina uweza wa kukosoa hilo. Ila ninamaanisha wimbo haujachapwa vizuri kwa kutumia 'Software'. Binafsi sipendi ku-review nyimbo ambazo hazijapangwa vizuri kwa sababu:

 • Nyimbo hizo huweza kumfanya mtu asivutiwe na wimbo (It repels), na hivyo mwisho wa siku kumfanya mtu asivutiwe na site.
 • Mtunzi yeyote, hatapenda wimbo wake usiwe katika hali ya kupendeza.

Je ni vitu gani vinavyofanya wimbo usiwe katika kiwango?

Kuna vitu vingi vinavyofanya wimbo usiwe katika kiwango. Na tukizingatia haya, basi tunaweza kuboresha site yetu.

 1. Watu wengi hawatenganishi Staff za kiitikio cha wimbo na mashairi. Hii hufanya kuwa ngumu sana kujua kama kiitikio kimeisha au la. Lakini pia kwa taratibu za muziki (mimi si mtaalam sana), sidhani kama ni sahihi.
 2. Kwa nyimbo ambazo mashairi huimbwa tofauti, wengine huunganisha mwisho wa shairi moja na mwanzo wa shairi lingine.
 3. Maneno ya wimbo hufichwa na nota, au nota hufichwa na maneno ya wimbo.
 4. Rest mahali ambapo hapatakiwi kuwa na rest (Nadhani software ya musescore in tatizo kidogo 'bug' inayosababisha hili).
 5. Ninakaribisha sababu nyingine ambazo labda mimi nimezikosa.

Je tufanyaje kuboresha kiwango cha nyimbo?

Well, kuna njia nyingi unazoweza kutumia:
 1. Tafuta msaada kupitia Google. Mfano, waweza kusearch 'Formatting Songs in MuseScore' au 'Formatting Songs in Capella' nk. Hii itakupa muongozo wa jinsi ya kuboresha nyimbo.
 2. Tumia help ya 'software'. Mara nyingi mambo yote tunayohitaji kujua yapo 'well documented' kwenye help section ya software.
 3. Ukishindwa, omba msaada kwa anayeweza zaidi. 

Mimi naamini yafuatayo:

 1. Hamna anayependa wimbo wake usiwe katika hali nzuri ya utanashati.
 2. Hamna anayependa wimbo wa Mtunzi mwingine "Mf. Mgandu" usiwe katika hali ya utanashati.


Basi, katika imani hiyo, naomba tuweke jitihada zaidi katika kuboresha viwango vya nyimbo tunazoupload.