Swahili Music Notes imepata mabadiliko kadhaa.
Admin wetu, amekuwa katika mchakato wa mabadiliko haya kwa muda mrefu sana, kusema ukweli, muda mrefu kupita kiasi. Hii ni kutokana na changamoto mbalimbali alizozipata admin katika kufanya ya kazi hii. Matokeo yake, shughuli mbalimbali za ku-review nyimbo na nyimbo za Jumapili zililega. Lakini shukurani kwa Mungu kwa kuweza kufanikisha yote, maana kama yote yataenda sawa, basi changamoto za kuchelewa kwa nyimbo na ku-review, zitapungua kwa kiasi kikubwa.
Mabadiliko yaliyofanyika:
Shukrani:
Tutoe neno la shukrani kwa watumiaji wote wa SMN kwa matumizi yenu ya website hii na mawazo mengi mliyotoa. Mawazo mengi ambayo yamefanyiwa kazi, ni mawazo ambayo yametoka kwenu. Yalikusanywa kwa pamoja na kufanyiwa kazi.
Tazama video hizi ili ufahamu zaidi:
Ukurasa mpya wa nyumbani:
Fahamu kuhusu Category na Nyimbo:
Muonekano wa SMN kwenye simu
Watunzi na ukurasa wa mtunzi
Nyimbo za Jumapili
Wafahamu Uploaders
Jinsi ya ku-upload nyimbo