Ingia / Jisajili

Nafasi na Kazi ya Conductor by Richard Mloka [Sehemu ya Kwanza]

TUJADILI KWA UFUPI NAFASI NA KAZI YA CONDUCTOR

Awali naomba niwatake radhi kwa kuendelea kutumia neno ‘conductor’ mpaka sasa nimeshindwa kupata tafsiri yake kwa Kiswahili. Najua wengine wanamwita ‘mpimishaji’ na wengine’ mwongozaji’ au ‘mwimbishaji’. Naomba niendelee kutumia neno ‘conductor’ ili niwe huru kidogo.

Conductor ni kiongozi wa kundi la wanamuziki anayewakilisha uwajibikaji (responsibility) na mamlaka(authority). Tendo analofanya ni sanaa ya kuongoza na kuelekeza upigwaji/uimbwaji wa muziki kwa kutumia ishara zinazoonekana wazi (visible gestures). Kimsingi, wajibu wa conductor ni:

1. kuwaunganisha wanamuziki

2. Kuweka mwendo sawa (set the tempo)

3. Kuongoza maandalizi na mapigo

4. Kusikiliza kwa umakini (critical listening)

5. Kuunda/kutengeneza (shape) sauti za kundi linalopiga muziki.

Conuctor hupatikana katika bendi za muziki wa concert, orchestra, kwaya na makundi-unganishi ya muziki ( musical ensembles). Conductor kwa kawaida hushika aina ya fulani ya fimbo nyembamba nyeupe katika mkono mmoja kiitwacho ‘baton’ kwa ajili ya kuonesha mwendo na mapigo na mkono mwingine huutumia kwa vielelezo. Hata hivyo conductor anaweza kuongoza bila baton.

Itaendelea…………….