Ingia / Jisajili

Nafasi na Kazi ya Conductor by Richard Mloka [Sehemu ya Tatu]

Inaendelea... Kama haujasoma sehemu ya kwanza, tafadhali bofya hapa > http://www.swahilimusicnotes.com/page/nafasi-na-kazi-ya-conductor-by-richard-mloka

Kama haujasoma sehemu ya pili, tafadhali bofya hapa > http://www.swahilimusicnotes.com/page/nafasi-na-kazi-ya-conductor-sehemu-ya-pili-by-richard-mloka

Kabla sijaendelea mbele kuelezea sifa na wajibu wa conductor nimeona niongelee hapa mazingira ya kwaya zetu. Kilichonisukuma kufanya hivi ni maoni ya wadau wale walioandika kuwa hapa kwetu basi hatuna conductors wa kweli. Mazingira yetu ni tofauti. Nitajadili. Mazingira yetu ya kwaya zetu ni magumu mtu kuwa mkamilifu kwa 100% ya conductor mzuri , hata kwa 75%! Kwa sababu

  1. Kwaya ndizo zenye jukumu la kuongoza waumini katika uimbaji kwenye Misa na Ibada mbali mbali. Misa moja inaweza kuwa na uhitaji wa nyimbo 15 (makisio ya chini) na zote zinaongozwa na kwaya. Muda wa kupitia nyimbo (pieces) nzuri za classical au zenye ufundi mkubwa hakuna. Wanaoziimba wanajua wenyewe jinsi jitihada ya ziada ilivyofanyika. Madhehebu mengine kwaya si kiongozi wa nyimbo. waumini wote wanaimba kwqa kutajiwa namba ya wimbo, organist anaanzisha kisha kanisa zima wanafuata huo wimbo. kwaya ina sehemu yake inaitwa na kuimba ujumbe wao. mara nyingi ni wakati wa sadaka na meza ya Bwana (Komunyo). Hapo kwaya inaweza kujianda vizuri zaidi kwa vile wana nyimbo 2 tu kwa ibada nzima.
     
  2. Kwaya zinaweka nyimbo mpya kila Dominika. Katika Misa kwaya haiwezi kukwepa Wimbo wa mwanzo, Katikati, Shangilio na Wimbo wa Komunyo. Hizi ni kama mpya kwa sababu kuna mwaka A, B na C (bila kutaja sherehe katika kalenda ya kanisa) zinakumbushwa kwa namna ya kufundishwa tena na pengine zinatungwa mpya. Muda unakuwa mdogo kupitia mambo ya kiufundi katika nyimbo zetu. Ndio maana kuna neno "ku-brush". hata muda wa kunoa sauti (vocal training) hatuna.
     
  3. Wingi wa nyimbo, tuseme 20, katika Misa unaweza kumfanya conductor asahau Alama ya wakati (Time signature) katika baadhi ya nyimbo, akajikuta 4 4 anaongoza kama 2 4, 3 8 anaongoza kama 6 8. Nyimbo ni nyingi kukumbuka kila kipengee cha dynamic na expression. Kwenye tamasha ni raihisi kwa sababu huwa hazizidi nyimbo tatu kwa kila kwaya.
     
  4. Elimu ya muziki. Narudi pale pale, mbali ya kuwa baadhi ya conductors hawana elimu sahihi ya muziki lakini hata wapiga ala pia mfano wapiga ngoma. Kila mara nasikia upigaji wa ngoma wa 3 4 hautofautishwi na 6 8. Ngoma ndio inayotupatia rhythm na bahati mbaya wapigaji wengi wa siku hizi hawajui pigo la mkazo (accent beat) wanashabikia kuchanganya zile ngoma ndoigo kwa muda mrefu bila kupiga ngoma yenye pigo kubwa. Natamani siku moja nifanye workshop na wapiga ngoma! Mpiga ngoma asiyejua Alama ya wakati atatofautishaje upigaji kati ya wimbo na wimbo?
     
  5. Shughuli za maisha. Wanakwaya si watu wanaoimba kama professionals ( kukidhi mahitaji ya maisha kwa uimbaji tu) bali ni watu wanaojishughulisha na ajira, kilimo, biashara au masomo. Wanakuja kuimba mara tu baada ya kumaliza shughuli hizo -mazoezi yanachelewa. Anaweza kuwepo katika mazoezi kimwili lakini kifikra hayupolabda kuna tatizo kazini au nyumbai - utafundisha lakini hashiki kiurahisi. Siku unayomtegemea yeye amebanwa na kazi inayomletea mkate wake wa kila siku - performance itashuka kiwango au itaharibika. katika baadhi ya parokia nilizotembelea nimekuta wanamaliza mazoezi saa 12:30 jioni. Walianza saa ngapi? 11:45! kwa muda huo utapitia nyimbo ngapi kwa ufasaha zaidi?
     
  6. Mazoea: Kila jumapili mtu anaimba, anazoea na kuona kuimba ni kitu cha kawaida kiasi kwamba huhitaji mazoezi, tofauti na tamasha ambapo halifanyiki kila jumapili na hivyo watu kujiandaa sana kwa tukio hilo. Ndio maana ninapenda sana parokia zinazofanya tamasha walau mara moja kwa mwaka, inasaidia kuondoka katika uimbaji, uongozaji na upigaji wa nyimbo kwa mazoea. 

Kwa ujumla niseme tu, tuwatumie waliopo na tuwape moyo katika kujitolea kwao. Tuwaelekeze kwa unyenyekevu kule wanakopaswa kwenda iwe ni elimu au ujuzi zaidi wa muziki. Itaendelea...