Ingia / Jisajili

Swahili Music Notes yafikisha Nyimbo 2,000

Swahili Music Notes ilizaliwa tarehe 1 Disemba, 2011 na nyimbo takribani 5 hivi. Ilifikisha nyimbo 100 tarehe 9 January, 2012.  Ilipofika tarehe 21 Juni, 2012 (Siku ya Muziki duniani) tulifikisha nyimbo 500. Nyimbo 1,000 zilifikiwa tarehe 26, Septemba 2012. Na leo hii tunasherehekea nyimbo 2,000. 

Hongereni kwenu nyote. Wote wanaotembelea website na kuomba nyimbo kila siku mmesaidia kukuza website yetu. Wote mnao-'upload' nyimbo kila wakati, mmekuwa wawezeshaji wakubwa sana wa Website hii. Kwa kweli Swahili Music Notes isingekuwa na mafanikio makubwa kama haya kusingekuwepo mchango wa kila mmoja wetu. Hongereni sana na Mungu azidi kuwabariki.

Tunaposherehekea mafanikio haya makubwa, tuchukue muda tuangalie changamoto mbali mbali ambazo Swahili Music Notes inazipata:

  • Bado mwamko wa watunzi binafsi ku-upload / kutuma nyimbo zao ziwe uploaded ni mdogo.
  • Bado kuna idadi kubwa ya nyimbo ambazo zinatafutwa lakini hazijapatikana.
  • Bado kuna idadi kubwa ya nyimbo zinazoombwa ambazo zipo tayari kwenye website. Wahusika hawa-search vizuri.
  • Bado kuna nyimbo zina makosa, watunzi (walio hai) hawazikagui nyimbo zao. Pengine wengine hawana taarifa juu ya Swahili Music Notes au hawatumii kabisa internet.
  • Bado ukubwa wa kazi nyingi za ku-maintain website unamwangukia mtu mmoja tu. (Hili linafanyiwa kazi taratibu).
  • Bado website haijaweza kujitegemea kifedha ili iweze kufanikisha baadhi ya mipango yake kama kujitangaza na kujiboresha.
  • Bado website inajulikana na watu wachache mno.
  • Nyimbo za kila Jumapili hazitumwi kila wiki.
  • Search bado haijatengamaa.
  • Na nyinginezo...

Napenda kuamini kuwa changamoto hizi zote zitaweza kufanyiwa kazi kwa pamoja. Mawazo, maoni na mapendekezo yanaendelea kufanyiwa kazi. Wakati mwingine mawazo mengine yanachelewa kujibiwa au kufanyiwa kazi kutokana na kukamatwa kikazi kwa Administrator. Nitaendelea kuhakikisha kuwa yote mazuri yanatekelezwa.

Kwa sasa, Tusherehekee sote kwa Pamoja kufikisha nyimbo 2,000. Mungu awabariki. Hureeeee!