Ingia / Jisajili

The Power of the Swahili Music Notes Dashboard

Wengi wenu hamjatambua bado uwezo wa Swahili Music Notes Dashboard. Nachukua nafasi hii leo kuwaelimisha japo kidogo kuhusu Dashboard. Hii ni kwa faida kwa wanaopanga ku-upload nyimbo na walioupload nyimbo hapo awali.


Mambo unayoweza kufanya kwenye dashboard:

1. Una uwezo wa kuona nyimbo zote ulizowahi ku-upload kwenye Swahili Music Notes
 

  • Utaona nyimbo zilizohakikiwa (Reviewed)
  • Na ambazo hazikuhakikiwa, hivi karibuni, utapata nafasi ya kuona pia kwa nini nyimbo hazikuhakikiwa.

2. Una uwezo wa kupakia (upload) nyimbo mpya.

3. Una uwezo wa ku-edit wimbo na kufanya yafuatayo:

  • Kubadili jina la wimbo
  • Kubadili jina la mtunzi
  • Kuongeza ni tarehe gani na wapi wimbo ulitungwa
  • Kuongeza lyrics za nyimbo.
  • Pia unaweza kubadili pdf (kama unayo nyingine bora zaidi).
  • Pia unaweza kubadili au kuongeza midi file kama haikuwepo.


Hayo ndo mambo unayoweza kufanya kwenye Swahili Music Notes Dashboard, natumaini Beatus Idama na Augustine watakuwa ni mashahidi wangu.