Ingia / Jisajili

Mashamba Maximillian K. Mbj

Mfahamu Mashamba Maximillian K. Mbj, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Dar Es salaam Parokia ya Bikira Maria Consolata Kigamboni

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 63 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Dar Es salaam

Parokia anayofanya utume: Bikira Maria Consolata Kigamboni

Namba ya simu: 0752657198 / 0682912668 /0673181630

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

 Mimi ni mzaliwa wa Jimbo kuu la Mwanza Parokia ya Familia Takatifu Pasiansi Mwanza,

Kwa sasa ni  Mwanafunzi katika chuo cha Usimamizi wa Fedha, Nimesoma Montessori Primary school Mwanza,  St Pius X seminary Makoko Musoma Mara(SECONDARY) , Nsumba Boys High school Mwanza (HIGH SCHOOL),

Naishi kigamboni katika parokia ya Bikira Maria Wa Consolata.

Ni mwalimu wa kwaya pia nacheza kinanda kwa kiwango changu cha kawaida kabisa.

Napenda kujifunza sana Muziki kwaundani ili niweze kuutumia vyema katika jamii na kanisa la Mungu kwa ujumla.

Katika tasnia ya kujifunza kwangu Muziki nilianza kujifunza nikiwa Kidato cha pili na walimu wangu walikuwa ni

                                   i. Abel Jipili ambaye kwa sasa ni Frt akielekea Daraja takatifu la upadre

                                   ii.Peter respicious Magala

                                   iii.Steven Luhende

BAADA ya  kumaliza kidato cha NNE nilikutana na FE NYANZA ambaye alifanya jitihada kubwa sana kwangu mpaka sasa THOBIAS MORA, MATTHIAS MSAFIRI, BENEDICT MAGILU, JOSE NKUBA, LEONARD CHEYO

Kwakiasi kikubwa walinifundisha mengi sana kwa hatua waliyo kuwa nayo nikaweza kuanza kusoma nyimbo za kwenye kitabu cha NL

Katika kupiga kinanda nilikuwa na walimu ambao walinitoa sifuri mpaka hapa nilipo akiwamo DIONIZ MBILIZI, TIMOTHEUS MOPHAT SULLUSI, ERIC MALEZA, Na baada ya hapo ndipo nilipo kutana na MARINE MUTONGORE ambaye pia kwakiasi kikubwa sana huwa siwezi kumsahau kwani alinirekebisha pale nilipo kuwa ninakosea namshukuru pia GABINUS KASIGWA, FE NYANZA NJUNGANI kwakutoa muda wao na kunisikiliza pale nilipo kuwa nawauliza  

Pia nina watu ambao wamenijenga kuweza kucheza nyimbo ngumu hata pale nisipo jiamini wakanifanya nianze kujifunza kutunga nyimbo za hivyo ili nijijenge zaida ALAN MVANO, PROCES FAIDA, ambapo mpaka sasa hivi naweza kidogo ingawa sijafika sehemu ambayo ninaihitaji

Watu ninao wakubali katika tasnia ya Muziki wa kanisa na pia matamasha ambao ningependa kuzidi sehemu waliyopo ingawa changamoto ni nyingi ni pamoja na INNOCENT MUSHI, HEKIMA MINDE RAYMOND, NERIUS MUTONGORE, MARINE MUTONGORE, PASCHAL GUNGA, RONALD NAKAKA,

Watunzi ninaowapenda nakufuatilia nyimbo zao kwa sasa ni FE NYANZA, DB WASONGA, E OGEDA, BEATUS IDAMA, BE MAGILU, INNOCENT MUSHI.

Watunzi wa zamani ni MB SYOTE, JOHN MGANDU, JOSEPH MAKOYE, GF KAYETA, MALEMA na wengine wengi ambao wanazidi kunijenga pale ninapo kutana na nyimbo zao.

MUZIKI UNAZIDI KUKUA KILA SIKU NA WATU WENGI SANA WANAFIKIRI SANA KUJA NA KITU KIPYA AMBACHO KITAWAFANYA WAONE KANE NA MCHANGO MKUBWA SANA KATIKA MUZIKI.