Ingia / Jisajili

Magere E Nswasya

Mfahamu Magere E Nswasya, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Shinyanga Parokia ya Mwadui

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 66 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Shinyanga

Parokia anayofanya utume: Mwadui

Namba ya simu: 0782110280

Soma Historia na maelezo yake hapa

Historia / Maelezo

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwanza kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kumtumikia kwa njia ya uimbaji. Ndoto ya uimbaji ilianza nikiwa mdogo sana kabla hata ya kuanza kusoma shule ya msingi. Kwani niliteuliwa na wazazi wangu kuwa natumbuiza nyimbo pindi tulipokuwa tukipata wageni nyumbani, siku mgeni akifika baada ya chakula cha usiku niliambiwa niwakaribishe wageni kwa nyimbo. Na siku ya kuondoka kama kawaida niliwaimbia wimbo wa kuondoka. ilifikia hatua tukapata kwaya ya Familia ambayo iliwaburudisha wageni wa familia, mimi nikiwa Mwalimu wa kwaya hiyo. Kwa kipindi hicho sikujua Mungu ameniandaa kumuimbia.Nilipo anza shule ya msingi nilijikuta naendelea kuwa muimbaji wa kwaya ya shule. Baada ya hapo nilipo fika darasa la tano nilijiunga na kwaya ya Mt. Gregory Parokia ya Mt.Maria Kagunguli wilayani Ukerewe,, kwa kipindi hicho tulikuwa Jimbo kuu la Mwanza. Kwa sasa ni jimbo la Bunda. Baada ya kuhitimu masomo nilihamia wilaya ya Sengerema na kujiunga na kwaya ya Mt. Maria Kigango cha Kakobe hapo ndo nilipoanza darasa la mziki Mwalimu wangu akiwa Evarist Felecian Ndaki. Kwa sasa ni marehemu Mungu amjalie pumziko la milele. Nimshukuru sana Mwalimu wangu wa pili Ndg Salvatory William Mabula kwa mchango wake mkubwa bila kumsahau Mwl. Thobias Aluma ambae alinitia moyo na kunikazania hadi nikaweza kusimama na kufundisha nyimbo bila msaada wowote. Hapo ilikuwa mwaka 2004. Niliendelea kufundisha kwaya hiyo ya Mt. Maria hatimae nilichaguliwa kuwa Mwalimu wa kwaya ya shirikisho Parokia ya KALEBEJO Jimboni Geita. Tulisaidiana na walimu wa vigango mbali mbali ndani ya Parokia ya Kalebejo walipo hitaji msaada wangu. Kwa kipindi hicho hatukuwa na organist Kigangoni kwetu japo tulijitahidi tukanunua kinanda lakini kukitumia hadi tupate Mwalimu wa kukodi hasa wakati wa sikukuu au tunaenda ziara baada ya tukio hilo kinanda kinatunzwa. Hicho kinanda kilitumika hivyo hivyo hadi kikaharibika.Hiyo hali kwa upande wangu binafsi iliniumiza sana kuwa na kinanda lakini hatuwezi kukitumia hadi kimekufa!!!! Mwaka 2008 tulinunua kinanda kingine ndipo nikaamua kutoa maoni tupate Mwalimu wa kinanda tulimchukua Mwl. Benjamin Augustino (Kasegese) na akaja kutufundisha. Kati ya wanafunzi 14 tulio faulu kucheza japo kwa kuongoza uimbaji Kigangoni kwetu ni watatu tu. Akiwemo Gabriel Paull Zihabhandi, pamoja na Thomas John Masele. Baada ya hapo mwaka 2011 nilihamia Mwanza kikazi na kujiunga na kwaya ya Familia Takatifu Kigango cha Nundu kama Mwalimu, kwa sasa ni Parokia. Nilikaa kwa muda wa miezi 8 tu na kuhamishiwa kisiwani Zilagura sikukuta kwaya japo waimbaji walikuwepo lakini hawakuwa na Mwalimu baada ya kufika Jumapili tulipomaliza kusali ilitolewa nafasi ya kujitambulisha wageni sikupenda kusema kuwa ni Mwalimu wa kwaya kutokana na majukumu yangu na changamoto zake. Lakini nilishangaa mama mmoja aliniambia nisitoke mbele alikuja akasema mbele ya waumini akiwaomba wanakwaya wahuzurie mazoezi kwani huyu mgeni namtambua ni Mwalimu na Organist hivyo tumshukuru Mungu kwa kumleta hapa. Sikuwa na jinsi ilibidi nianze zoezi rasmi na kufuata ratiba ya mazingira yale na kwaya ilifanya vizuri. Mwaka 2013 ndipo nilipohamia Jimbo la Shinyanga na kufanya huduma ya uimbaji Mwalimu wa kwaya ya Mt. Stephano shahidi na Parokia kwa ujumla. Kanisa la Msalaba Mtakatifu Parokia ya Mwadui. Hadi leo nafanya kazi ya utume wa uimbaji hapa Mwadui. Natoa shukrani zangu kwa Mwalimu kiongozi wa kwaya ya Mt. Stephano Mr. Joseph Bazil , pamoja na Mwl. John Somi, Mwalimu kiongozi wa shirikisho Parokia na jimbo kwa ushirikiano na msaada mkubwa walio nisaidia hadi leo. Tumuimbie Bwana katika roho na kweli. Nazidi kutoa shukrani kwa walimu wote wanao endelea kunisaport katika kuelekezana mambo mbalimbali katika mziki na katika utume ki ujumla mbarikiwe sana.