Mfahamu Paschal Lusangija, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Morogoro Parokia ya MT.MONIKA KIHONDA MOROGORO
Idadi ya nyimbo SMN: 127 > Zitazame
Jimbo analofanya utume: Morogoro
Parokia anayofanya utume: MT.MONIKA KIHONDA MOROGORO
Namba ya simu: 0782402378/0743402378
Soma Historia na maelezo yake hapaWasiliana na mtunzi kwa email:
Paschal Lusangija Nyanda amezaliwa mwaka 1988,mwezi wa kwanza tarehe 8 katika Kijiji Cha Zomadi kata ya China Cha Nkola wilaya ya Igunga mkoani Tabora.Amesoma shule ya msingi Chibiso na kufaulu kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Mwisi.Baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato Cha 5 na 6 katika shule ya wavulana Umbwe iliyopo kibosho mkoani Kilimanjaro.Alipomaliza alichaguliwa kujiunga na masomo ya chuo kikuu Cha kilimo sokoine mkoani Morogoro katika shahada ya Elimu akichukua masomo ya jiografia na baiolojia.