Mfahamu Sebastian G. Fuluge, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Iringa Parokia ya Ilole
Idadi ya nyimbo SMN: 16 > Zitazame
Jimbo analofanya utume: Iringa
Parokia anayofanya utume: Ilole
Namba ya simu: 0757364250
Soma Historia na maelezo yake hapaWasiliana na mtunzi kwa email:
Sebastian G. Fuluge ni Mwalimu kiongozi wa kwaya kuu ya Bikira Maria Afya ya Wagonjwa iliyoasisiwa mnamo mwaka 2003. Sebastian G. Fuluge amekuwa maarufu katika tasinia ya utunzi WA nyimbo za kanisa ndani na nje ya nchi hasa kwa wimbo wake unaopendwa na watu wengi sana hapa Tanzania, Kenya na nchi nyingine wimbo maarufu kama "Baba tunaleta vipaji". Ni mtoto WA tatu kati ya sita kutoka familia ya Mzee Gaudence Mustafa Fuluge na Bibi Maulisia Peter Mfalamagoha. Alizaliwa tarehe 31 . 05 . 1975 katika kitongoji Cha Madukani, Kijiji Cha Kitumbuka, wilaya ya Kilolo, mkoa WA Iringa. Na kwa Sasa anaishi kitongoji Cha Vigulu, Kijiji Cha Ilole, wilaya ya Kilolo, mkoa WA Iringa.