Mtunzi: Thadeo Mluge
> Mfahamu Zaidi Thadeo Mluge
> Tazama Nyimbo nyingine za Thadeo Mluge
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Matawi
Umepakiwa na: Thadeo Mluge
Umepakuliwa mara 11 | Umetazamwa mara 23
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Antifona / Komunio Dominika ya Matawi
MAPENZI YAKO YATIMIZWE.
Ee Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kiniepuke (sio) kama nitakavyo mimi (ila) mapenzi yako yatimizwe.x2
1. Yesu akaenda na wanafunzi wake, mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia Ketini hapa, niende nikaombe.
2. Akawachukua Petro na wale wawili ambao ni wana wa Zebedayo, akawaambia, Roho yangu inahuzunika kwa kiasi cha kufa.
3. Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.
4. Tena akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? Kesheni, na muombe, msiingie majaribuni; kwa maana roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.