Ingia / Jisajili

Dr. David S. Kacholi

Mfahamu Dr. David S. Kacholi, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Dar es Salaam Parokia ya St. Francis Xaviery, Chang'ombe - Dar es Salaam

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 98 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Dar es Salaam

Parokia anayofanya utume: St. Francis Xaviery, Chang'ombe - Dar es Salaam

Namba ya simu: +255754471178

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Ni mwimbaji, Mtunzi na Mwalimu wa kwaya.

Kwaya nilizoimbia: Kwaya ya Vijana (Parokia ya Upanga), Don Bosco (Temeke Mikoroshini), SUA-Mazimbu (Morogoro), Mt. Augustino (Parokia ya Chang'ombe), na Mt. Francis Xavier (Parokia ya Chang'ombe).

Kazi: Mhadhiri (DUCE - Idara ya Sayansi ya Viumbe Hai)

Elimu ya Muziki: Elimu ya kusoma muziki na utunzi nimeipata kwa watu mbalimbali na kwa vipindi mbalimbali pale nilipoweza kuwafikia walimu na watunzi wazoefu. Kwa upekee Br. Pius Nkilagomva ndiye aliyeniamasisha kujifunza muziki wakati nikiwa Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili -Upanga, Mr. Constantine Chambala ndiye aliekuwa mwalimu wangu wa kwanza kunifundisha do,re, mi fa, so, la, ti, do, Mr. Stanslaus Mujwahuki, Mr. John Mgandu na Mr. Sabinus Komba wamenisaidia kwa kiasi fulani kujifunza Music Harmony and Composition. Pamoja na kuwashukuru walimu niliowataja hapo, sehemu kubwa ya elimu yangu ya muziki nimekuwa nikiipata kwa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyohusu Composition, Harmony, Modulation, n.k. Pamoja na uelewa kiasi wa muziki nilionao, bado napenda kujifunza zaidi toka wale wenye uelewa mpana wa somo la muziki mtakatifu. Pia nakaribisha wote wenye kupenda kubadilishana nami uzoefu katika muziki mtakatifu. Tumsifu Yesu Kristu,.....

Current Address: Yombo Vituka Plot 425, P. O. Box 45926 Dar es Salaam

E-mail address: kacholi78@yahoo.com