Ingia / Jisajili

Derick Nducha

Mfahamu Derick Nducha, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Kuu Katoliki la Mbeya Parokia ya Mlowo

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 121 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Kuu Katoliki la Mbeya

Parokia anayofanya utume: Mlowo

Namba ya simu: +255746221933/+255627697152

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Tumsifu Yesu Kristo.....!! Naitwa Derick Oscar Nducha, Ni mzaliwa wa Mlowo Mbozi mkoa wa Songwe. *HISTORIA YA MUSIC MTAKATIFU* Nilianza kufundishwa kucheza kinanda mwaka 2011, na Baba yangu mzazi Oscar E.Nducha, nikiwa Darasa la Saba, Mwaka 2012 nilianza kucheza kinanda baadhi ya nyimbo kanisani, Mwaka huohuo mwezi wa 12, nilianza kujiamini nikawa nacheza mpaka Misa yote, katika kwaya ya MT Monica Mlowo Madukani, Mwaka 2013 Mzee Nducha akanipa maagizo niwe Muhudumu wa kwaya hiyo Mt.Monica ,wakati huo yeye akihudumu kwaya zingine Mt.Agustino, & Mt, Secilia na zingine Vigangoni, Mwaka huo Mzee Nducha akanipa Mafunzo ya awali ya Music wa Notes, mpaka alipoishia yeye(Utambuzi wa Staff G & F cleff, Funguo, na Thamani za notes) Baadae ya hapo alikuja Mwl.Andrea Mwashibanda yeye alikuwa SI mtaalamu wa kucheza kinanda kwahiyo ikabidi tubadilishane nikampa Mafunzo kadili nilivyofundishwa naye kaniendeleza mpaka nikajua, Mwaka 2014 Mwezi wa 12 nilianza kutunga nyimbo na wimbo wakwanza ulikuwa ni ENYI WATU WA SAYUNI. Upo kwenye Tovuti. Karibu uungane nami katika kuutangaza Utukufu wa Mungu. ??