Ingia / Jisajili

Deus V.Chicharo

Mfahamu Deus V.Chicharo, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la DAR ES SALAAM Parokia ya CHAMAZI

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 86 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: DAR ES SALAAM

Parokia anayofanya utume: CHAMAZI

Namba ya simu: 0758003914

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Deus Vitus Chicharo alizaiwa katika kijiji cha Mkongoro katika mkoa wa kigoma tar 11/12/1991.Akiwa na umri wa miaka miwili wazazi wake walihamia katika kijiji cha Songambele kilichopo katika wilaya ya uvinza mkoani kigoma.Mwaka 2001 aliandikishwa katika shule ya msingi Songambele na kuanza kusomea hapo.Mwaka 2005 aliamishiwa katika shule ya msingi iligala iliyopo katika wilaya hiyo na mnamo mwaka 2007 alimaliza masomo yake ya elimu ya msingi na akachaguliwa kujiunga na shule ya upili katika tarafa hiyo ya Ilagala.Alisoma hapo katika shule hiyo na kuhitimu masomo ya sekondarimnamo mwaka 2011;Kutokana na changamoto za kimaisha hakufanikiwa kufaulu kwenda katika masomo ya juu hivyo akaamua kwenda katika jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kufanya biashara. MAISHA YA UTUME Deus Chicharo ni mtoto wa nne katika familia ya Katekista Vitus Chicharo yenye watoto (8)nane na mama Catheline Gabliely akiwa ndiye mama yake.Katika maisha yake ya utume wa uimbaji ni hadithi ndefu sana kwani hata mwenyewe anashangaa mahali hapa alipo kwa sasa kwakuwa hakupategemea kabisa kwamaana ndoto yake kubwa ilikuwa ni upadre lakini kutokana na uduni wa maisha ya wazazi wake hakuweza kwenda kusomea seminari kwani ada yake ilikuwa ni ghali ikilinganishwa na shule za serikali ambapo katika kipindi hicho ada ilikuwa ni shilingi 20,000/= Alianza kuimba katika kwaya ya watoto ''sunday school" mwaka 1998 akifundishwa na baba yake Vitus Chicharo,baada ya mwaka 2003 alijiunga na kwaya ya mtakatifu Bikira maria mama wa mungu iliyopo katika kigango cha Songambele parokia ya Sunuka jimbo katoliki la Kigoma na akaimba kwa kipindi kifupi chini ya mwalim Batromew Kahagwe.Baada ya kuhamishiwa katika kijiji cha Ilagala kwa ajili ya masomo Deus hakuendelea tena kuimba badala yake ndoto zake zikawa zimehamia katika utunzi wa nyimbo za kidunia yaani "Bongo fleva" taratibu alianza kujifua kwa nguvu ili aweze kuyatimiza malengo yake lakini mambo hayakuwa kama alivyo tarajia na alipoanza masomo yake ya sekondari aliachana na ndoto yake hiyo ya kuwa msanii na hatimaye akajiunga na kwaya ya vijana ya shuleni hapo yaani TYCS mwaka 2009.Kutokana na kuimba mziki wa kikatoliki Deus alivutiwa sana na muziki hata akashawishika kutaka kujifunza muziki lakini hakupata sapota kutoka kwa mwalimu aliyekuwa akiifundisha kwaya hiyo kwakuwa alikuwa akipendelea sana kuujua muziki tokea shule ya msingi nyuma aliona akijua muziki kwake itakuwa furaha kubwa kwani itamwea rahisi kutunga nyimbo. Baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne alirudi katika kigango chake cha Songambele na akapewa jukumu la ulezi wa watoto wa utoto mtakatifu.Aliwalea watoto hao kwa upendo pamoja na kuwatungia nyimbo pamoja na michezo mbalimbali ya watoto ambayo kwa kiasi kikubwa iliwaburudisha sana watoto aliweza kutunga nyimbo za kitamaduni na nyimbo za misa ingawa hakujua muziki.Kutokana na bidii zake za kuwalea watoto watoto wotez walimpenda sana na akaishi nao kama kaka yao. Waamini wakadhani ya kwamba sasa atakua katekista kupokea kijiti cha baba yake lakini haikuwa hivyo.Pia kutokana na utunzi wa nyimbo za kumsifu Mungu baadhi ya walimu na waimbaji wa kwaya wakaanza kumwita "Mukasa" wakati huo yeye hakujua mukasa ni nani au ni nini au hakujua wanaongelea kitu gani akawa anajiuliza mkasa..? mkasa gani..? alipouliza kuhusu Mukasa aliambiwa kuwa Mukasa ndiye mtunzi aliyetunga wimbo wa Yesu ni mwema,kidole juu,Tung'ang'aniye imani n.k" ambazo zilikuwa ni nyimbo zilizokuwa zikiimbwa sana kanisani kwao wakati huo.Kutokana na jina hilo la mtunzi huyo Deus alivutika sana na Bernard Mukasa hivyo naye akaanza kumpenda sana mtunzi huyo wa wa mziki wa kanisa katoliki nchini Tanzania. Mwaka 2012 mwalimu Erasto Petro maarufu kama "Paroko" aliyekuwa mwalimu kiongozi wa kwaya ya mtakatifu Bikira maria alimwambia Deus unajua kutunga nyimbo za kanisa ingawa hujui muziki ni vizuri ujifunze muziki ili iwe rahisi kwako katika kutunga nyimbo zako;Bila kuchelewa alianza darasa la muziki na kuendelea kujifunza kwa bidii na wakati huo alikuwa anaimba katika kwaya hiyo ya mt.Maria pamoja na kuwalea watoto wa utoto mtakatifu maarufu kama shirika la mtoto Yesu katika jimbo hilo.Na aliendelea na kujifunza kwa bahati mbaya alisafiri kwenda dar essalaam akiwa hajaiva kimuziki na alipofika jijini Dar alijiunga na kwaya ya Mt.Yosefu mfanyakazi iliyopo katika parokia ya Mt crala wa asizi Chamazi akiwa kama mwanafunzi wa muziki.Alizidisha juhudi zake za kujifunza na hatimaye Mungu akamfungulia milango mwaka 2013 akaanza kufundisha angalau kwa kiasi chake na na mwaka 2015 aliweza kutunga wimbo wake ambao ulikuwa na makosa mengi ya kiufundi taratibu hakuchoka akakazana kutunga nyimbo za kanisa mpaka angalau akaweza kidogo kuonesha mwanga wa matumaini.Tokea kipindi cha uanafunzi mpaka leo amefanikiwa kutunga nyimbo zaidi ya 200 na nyimbo kumi kati ya hizo zimerekodiwa katika kwaya tofauti tofauti. Deus Chicharo anapenda sana nyimbo za tafakari zinazogusa uhalisia wa kiimani pamoja na tafakari za maisha;pia anaimba sauti ya tatu maarufu kama tennor na anamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha ya utume huu ingawa una changamoto nyingi na kitu cha pekee sana anachokipenda kuliko vyote ni ndoto ya kuwa mtakatifu..... Deus anapenda sana maisha ya mtakatifu Rita wa kashia na ndiye mtakatifu anayempenda zaidi na mpaka leo Deus bado anafanya utume wake katika parokia ya Mt Crala wa asizi Chamazi jimbo kuu la Dar es saam....