Ingia / Jisajili

Emanoel Makata Apolinari

Mfahamu Emanoel Makata Apolinari, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Moshi Parokia ya Mkuu

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 43 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Moshi

Parokia anayofanya utume: Mkuu

Namba ya simu: 0620670272

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

UTANGULIZI:

Naitwa Emanoel Makata Apolinari. mzaliwa wa mkoa wa kilimanjaro wilaya ya rombo jimbo kuu katoliki la Moshi. nimesoma elimu ya msingi (Mharu) na sekondari (Shimbi na Mkuu) ndani ya Jimbo na elimu ya chuo kikuu Teofilo Kisanji University (TEKU) mkoa wa Mbeya jimbo kuu katoliki la Mbeya. nimeanza uinjilishaji kwa njia ya uimbaji kama mwalimu tangu mwaka 2010 nikiwa kidato cha nne.


Nimeoa na nina mke na watoto wawili hadi sasa 04/11/2019. 

Kwaya nilizoimba hadi sasa. Nimefanikiwa kuimba katika kwaya zifuatazo: kwaya ya familia takatifu Mkuu parokiani, Kwaya ya Mt. sesilia Mkuu, Mt, Brigitha Mkuu, kwaya ya shule shimbi sekondari, Shule ya sekondari Ungwasi, Shule ya sekondari Mkuu, Mt Augustino chuo kikuu TEKU Mbeya, Mt joseph kigango cha idodi Iringa, Mt. Joseph Parokia ya Kijenge Arusha, Mt sesilia Songwe Mbeya, Mt Kizito Makuburi Dar es salaam, Mt joseph Parkia ya Kanoni Karagwe Kayanga, Moyo Mtakatifu wa Yesu Rwambaizi Kayanga.

HITIMISHO:

Namshukuru sana Mungu alienipatia sauti ya kumwimbia, Nitamwimbia na kumsifu yeye peke yake. nawatakia utume mwema. tumsifu Yesu Kristu