Ingia / Jisajili

Ernest Magunus

Mfahamu Ernest Magunus, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la kahama Parokia ya kahama mjini

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 27 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: kahama

Parokia anayofanya utume: kahama mjini

Namba ya simu: 0759852211

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Ni mwimbaji, Mtunzi wa Muziki Mtakatifu na Mwalimu wa kwaya.

 
Kwaya nilizoimbia: Kwaya ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume (Parokia ya Kahama mjini), Mt. Maximilian corbel (Parokia ya Kahama Mjini), Kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu (Chuo Kikuu Dodoma), Mt. Teresia wa Mtoto Yesu (Parokia ya Matogoro – Songea), Mt. Lucia (Chuo cha Ualimu Songea STC).
 
Kazi: Mwalimu wa shule za sekondari kwa Masomo ya Physics na Mathematics.Historia ya utume wa uimbaji kwakifupi;
      Nimeanza utume wa uimbaji wa kwaya rasmi Mwezi wa kwanza 2008  Nikiwa na miaka 11 ya kuzaliwa katika Kwaya ya Wat. Petro na Paulo mitume (Parokia ya Mt Karoli Lwanga – Kahama mjini, Kigango Cha Bikiramaria Mkingiwa dhambi ya asili - Shunu ).  
      Nilianza kujifunza Muziki Mtakatifu 2014 ikiwa ni Miaka 6 tangu niaze utume wa uimbaji. Katika Uimbaji wangu nime fanikiwa kurekodi album mbili nikiwa na kwaya tofauti. Pia katika Muziki nimefanikiwa kutunga nyimbo kazaa za Dini. Kwa sasa na toa utume wangu nikiwa na kwaya ya Mt. Maximilian Corbel Kahama - Shunu,  nikiwa kama Mwalimu wa Kwaya hiyo.
 
Elimu ya Muziki: Elimu ya kusoma muziki na utunzi nimeipata kwa watu mbalimbali na kwa vipindi mbalimbali Kutoka kwa walimu na watunzi wazoefu. Kwa upekee Mwalimu Caroli Stephen wa Parokia ya Mt. Caroli Lwanga (Kahama Mjini ) ndiye aliyekuwa mwalimu wangu wa kwanza kunifundisha do,re, mi fa, so, la, ti, do, Mr. Jackson Paulo, Mr Sonda na Mr. Emmanuel wa Matogoro - Songea, wamenisaidia kwa kiasi fulani kujifunza Music Harmony and Composition pia Upigaji wa keyboard. Pia Kwanamna ya pekee na Mshukuru Adimn wa “Swahili Music Notes” kwa ushauri wake mzuri katika kuhakiki ubora wa Nyimbo (SMN) kwakweli Umenisaidia sana. Pamoja na kuwashukuru walimu niliowataja hapo, sehemu kubwa ya elimu yangu ya muziki ninaendelea kuipata kwa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyohusu Composition, Harmony, Modulation, n.k. Kutokana na Uwezo  Mdogo kiasi wa muziki nilionao, bado napenda kujifunza zaidi toka kwa wale wenye uelewa mpana wa somo hili la muziki hivyo napenda kukaribisha Ushauri na maelekezo mbalimbali unayoona una weza kunitoa sehemu hii nilipo nakunipa ujuzi zaidi katika muziki mtakatifu. Tumsifu Yesu Kristu,.....
 
Current Address:  Kahama - Shunu,  S.L.P 16 Kahama.

E-mail address: ernest.magunus1500@gmail.com, Phone: 0718354080/0759852211