Ingia / Jisajili

Dr Eusebius Jose Mikongoti

Mfahamu Dr Eusebius Jose Mikongoti, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Ifakara Parokia ya Mt. Augustino - Chita

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 6 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Ifakara

Parokia anayofanya utume: Mt. Augustino - Chita

Namba ya simu: +255719595486

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Mimi ni daktari wa magonjwa ya binadamu ambaye hupenda kumtumikia Mungu kwa njia za kutibu magonjwa na kufanya muziki Mtakatifu kwa njia za kuimba na kupiga kinanda. Falsafa ninayoiamini ni kuwa "Binadamu hutibu magonjwa lakini Mungu ndiye mponyaji"!

Pia katika taaluma yangu ya utabibu Kwa asilimia kubwa muziki unanisaidia sana katika kupata kile ninachokitamani kiwe Kwa wagonjwa ninao wahudumia.

Kuzaliwa na Elimu

Nimezaliwa tarehe 18/02/1987 katika kijiji cha Chita kilichopo katika wilaya ya Kilombero, mkoa wa Morogoro. Wazazi wangu ni; Hayati Mzee Joseph Mikongoti (1934 - 2008) na Bi Imelda Valimba (yuko hai mpaka sasa). 

Nimesoma katika shule ya Msingi Ching'anda (1996 - 2002) iliyopo kijijini Chita.

Mnamo mwaka 2003 nilijiunga na seminari ya swali ya Mtakatifu Patriki Sofi wilayani Malinyi Mkoa wa Morogoro.

Miaka ya 2004 Hadi 2007 nilikuwa katika seminari ndogo ya Mtakatifu Fransisco iliyoko wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro. Hapo nilihitimu ya masomo ya cheti ya shule ya upili (Certificate of Secondary Education).

Mwaka 2008 mpaka 2010 nilipata masomo ya juu ya shule ya upili (Advanced education) katika shule ya Kibaha iliyoko Mkoani Pwani.

Nilisoma katika chuo Kikuu Cha Dodoma (2011/2014) na baadaye kuhamia Chuo Kikuu kishiriki cha Mtakatifu Fransisco Ifakara (2014/2017) katika kuendeleza safari ya kuitafuta shahada ya udaktari. Mnamo Mwezi November 2017 nilihitimu shahada ya awali ya udaktari wa magonjwa ya binadamu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Mtakatifu Fransisco Ifakara na kuzawadiwa cheti.

Maisha na Muziki

Marehemu Baba yangu, Hayati Mzee Joseph Mfaume Mikongoti ndiye aliyenihamasisha katika kutamani elimu ya muziki. Mzee huyu alikuwa akishirikiana na mke wake (yaani mama yangu) katika kutulea katika misingi ya muziki. Nakumbuka kipindi nipo mdogo (nadhani miaka ya 1992 hivi) pindi nimeanza kupata ufahamu, Marehemu Baba alikuwa anatufundisha nyimbo mbalimbali za kanisa mfano; Kwa mshangao tuwaze, Twakusifu Mungu Mkuu, Binadamu inama kichwa, Yosefu tunakutolea n.k. Kazi hii waliifanya Kwa ushirikiano mkubwa na mama. Nilikuwa nikiimba vizuri mama yangu alikuwa akinipa Zawadi ya ndizi za kuiva Kaka zangu alikuwa hawapatii Kwa kigezo cha kuwa "waliimba vibaya"

Kitendo cha uhamasishaji wa wazazi wangu niliona kuna kitu kilipungua katika muziki ndani ya familia yetu kwani Baba yangu hakujua nota wala Kinanda. Baba alikuwa anatufundisha na kumsifia Mzee mmoja aliyekuwa anaitwa Kingumwile (RIP). Huyu Mzee alikuwa ni muhudumu wa afya (sifahamu nafasi yake ilikuwa nini). Baba alikuwa anamsifia Sana Kwa kutuambia "Hizi nyimbo Dokta Kingumwile anazisoma vizuri kwenye nota na kuzipiga kwenye kinanda Safi sana"!  Hii kauli ilikuwa inanihamasisha Sana, katika hali ya utoto nilipata kuwaza "Kumbe ukitaka kujua nota na kupiga kinanda ni lazima uwe daktari"! Hapo ndipo ndoto zangu za kuwa mwanamuziki Mtakatifu na mpiga kinanda na udaktari zilipoanza. 

Kipindi nilipofaulu kujiunga na seminari ya swali ya Mtakatifu Patriki Sofi nilimuahidi Marehemu Baba kuwa "Lazima nitakuwa mpiga kinanda"  japo Kwa bahati mbaya nilipoanza masomo ya seminari sikubahatika kuchaguliwa kuwa mmoja wa vijana watakao jiunga na darasa la muziki! Iliniuma Sana! Niliona ndoto zangu za muziki zinakufa, nilijiona mimi ni muongo mbele ya Baba yangu! Hakika nilijiuliza "nitawajibu nini wazazi wangu?!"

Elimu ya muziki na ari ya kuwa daktari

Baada ya kumaliza mwaka mmoja katika seminari ya awali Sofi nilijiunga na seminari ndogo ya Mtakatifu Fransisco! Huko nilijipa moyo kuwa ndoto yangu ya kusoma muziki na kupiga kinanda itatimia. Kwa bahati mbaya Kwa mara ya pili Jambo hilo halikuwezekana tena! Darasani kwetu walichaguliwa wenzangu watatu; Paxdomine Mteketa (RIP), Chrisostom Ngalandwa na Jistanus Mkola! Lol! Nikaumia tena! Nikajisemea "Sitaki tena muziki" lakini hofu ilikuwa "nitawaambia nini wazazi?!" Kipindi nipo kidato cha Kwanza nilisoma kamusi fulani ya kutoa maana ya maneno ya kiingereza nilijikuta naangalia maana ya neno "Doctor"  ilichorwa picha ya kichwa cha mtu mwenye uwalaza (upaa)! Hakika niliutamani ule upaa, nikajisemea "Lazima niwe daktari"! Niliamsha Ari yangu ya mwanzo ya kuwa daktari kama Mzee Kingumwile aliyekuwa akisifiwa na Baba! Nikaendelea kukazana na masomo ya sayansi.

Kipindi nipo kidato cha tatu nikawa nawasumbua sana wale wanafunzi wenzangu waliochaguliwa kusoma muziki ili wanielfundishe! Marehemu Paxdomine alikuwa nanisaidia sana katika kujifunza muziki, pia Ndg Justine Mtafungwa aliyekuwa darasa moja mbele yangu alinisaidia Sana kunielekeza. Bila kuwasahau; Br Onesmo Sanga (OSB), Peter Mayombo na wengine hakika walinisaidia Sana pale Kasita Seminari Ulanga.