Ingia / Jisajili

Fausto C. Kazi

Mfahamu Fausto C. Kazi, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Jimbo Kuu la Dodoma Parokia ya Makole

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 19 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Jimbo Kuu la Dodoma

Parokia anayofanya utume: Makole

Namba ya simu: 0655543705/0755543705

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Tumsifu Yesu Kristo.......................

Fausto Charles kazi ni mwanakwaya wa sauti ya tatu katika kway ya Mtakatifu Gaspar Del Bufalo, Parokia ya Mt Gaspar Del bufalo Makole, Jimbo Kuu la Dodoma.

ELIMU YA MUZIKI.

March 2013 alijiunga na mafunzo ya muziki wa kanisa katika kanisa la KKKT usharika wa Dodoma mjini chini marehemu Mwl Malisa (Raha ya Milele umpe Ee Bwana, Apumzike kwa Amani Amina)  aliyekuwa mkufunzi wa mafunzo hayo. April 2014 alihitimu mafunzo kwa nadharia na vitendo ambapo mpaka sasa ni Mwalimu wa kwaya, mpimishaji, Mtunzi na mpiga kinanda. Kwa muda wa miaka 2 amefanikiwa kutunga nyimbo yapata 60 ambapo 9 kati ya hizo zimerekodiwa na kwaya tofauti tofauti ndani na nje ya Jimbo Kuu la Dodoma.

UTUME.

Katika utume wa wa uinjilishaji kwa njia ya kuimba, ametoa huduma katika kwaya zifuatazo.

1. Kwaya ya Mt. Paulo wa Msalaba -  Nzasa.

2. Kwaya ya Mt. Augustino wa Hippo- Swaswa.

3. Kwaya ya Mt. Cecilia - CBE-Dodoma.

4. Kwaya ya Kristu Mfalme - Kizota

5. Kwaya ya Mt Gaspar Del Bufalo -  Makole ambapo yupo hadi sasa.

Katika utume wake ameshiriki mashindano ya kwaya yaliyofanyika Dodoma katika hotel ya Mt Gaspar 2015 & 2016. Pia ameshiriki kazi ya kurekodi albam 7 za kusikiliza (Audio) ambazo ni:-

1. Alpha na Omega - Mt. Gaspar Del Bufalo - Makole.

2. Mtoto Yesu Amezaliwa - Mt Gaspar Del Bufalo - Makole.

3. Tuombee Miito - Mt. Cecilia - Isangha

4. Karibu kwetu Masiha - Mt. Gaspar Del Bufalo -  Makole.

5. Bwana Amenituma - Shirikisho Dekania ya Mt. Paulo wa Msalaba.

6. Nimeanza Kazi - Mt. Cecilia CBE - Dodoma

7. Enendeni Ulimwenguni - Shirikisho - Makole.

SHUKRANI.

Anamshukuru Mungu kwa kumjalia karama hii kwa ajili ya huduma ya kanisa na anaomba hekima ili aendelee kutumika bila kuchoka wala kukata tamaa. Kwa namna ya pekee anaushukuru uongozi wa KKT usharika wa Dodoma mjini kupitia Mwl Malisa kwa msaada wake wa maarifa na kujituma katika muziki ( nadharia na vitendo). Shukrani za pekee ziwaendee walimu owte waliomsaidia na wanaoendelea kuwa naye karibu kwa ushauri na kumpatia ujuzi wao.

1. Lucas  Masila

2. Justine salisali

3. Isaya Masawe

4. Joseph Waziri

5. Thomas Mwakimata

Mwisho anawashukuru wote waliomsaidia na wanaonendelea kumsaidia katika utume wake lakini hawakuorodheshwa katika profile hii anauthamini sana mchango wao na Mungu awabariki. Amina

KWAKO BWANA ZINATOKA SIFA ZANGU KATIKA KUSANYIKO KUBWA " ( MY PRAISE SHALL BE OF THEE IN THE GREAT CONGREGATION)