Ingia / Jisajili

Flavian Benedicto Kabebe

Mfahamu Flavian Benedicto Kabebe, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la KAYANGA Parokia ya RWAMBAIZI

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 8 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: KAYANGA

Parokia anayofanya utume: RWAMBAIZI

Namba ya simu: 0622031286

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

UTANGULIZI:

Mimi naitwa mwalimu Flavian Benedicto Rwabwigamo, nilizaliwa tarehe 27/01/1990 Kijiji cha Rwambaizi kata ya Kanoni, Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Nilipata elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Rwambaizi, elimu ya sekondary katika shule ya sekondari Rwambaizi.

UTUME WA UIMBAJI.

Mnamo mwaka 2008 mwezi wa pili nilijiunga na kwaya ya Moyo mtakatifu wa Yesu Parokia ya Rwambaizi. Mwaka 2012 Nilianza mafunzo ya muziki ndani ya kata ya Kanoni kwa bwana Symberity, parokia ya Rwambaizi, Nikaanza kufundisha kwaya mwaka 2014, Kwaya ya Kristu mfalme Kigango cha Nyamalembo Geita mjini.

KWAYA NYINGINE NILIZOHUDUMU NI KAMA IFUATAVYO:

MT. JOSEPH Kagera sugar camp5 parokia ya Kashambya jimbo la Bukoba, Mt. sesilia kigango cha Ilemela MUleba Jimbo la Bukoba parokia ya Kijwile, Mt. Lusia kigango cha Bulembo Parokia ya Kashambya Jimbo la Bukoba, Mt. Joseph Parokia ya Kanoni Kayanga Kagera, Mt Francisco kigango cha Kibona Kayanga, Kwa sasa kwaya ya Moyo mtakatifu wa Yesu parokia ya Rwambaizi Jimbo la Kayanga na nyingine kadhaa