Mfahamu Furaha Mbughi, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Jimbo Katoliki la Mbeya Parokia ya Parokia ya Igogwe
Idadi ya nyimbo SMN: 146 > Zitazame
Jimbo analofanya utume: Jimbo Katoliki la Mbeya
Parokia anayofanya utume: Parokia ya Igogwe
Namba ya simu: 0758 972025 / 0786 847120
Soma Historia na maelezo yake hapaWasiliana na mtunzi kwa email:
Tumsifu Yesu Kristu.
Furaha Mbughi ni mtunzi na mpiga kinanda mchanga.
Napenda sana kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Namshukuru Mungu kwa karama alizonijalia.
Nilianza kuimba kwaya mwaka 1994 katika Kigango cha Mt.Athony, Kafwafwa, Parokia ya Sange, Jimbo la Mbeya.
Miaka 10 baadaye, yaani mwaka 2004, nilianza kujifunza muziki wa nota na kucheza kinanda, wakati huo nikiwa kidato cha tano katika sekondari ya wavulana ya Mzumbe. Na kwa mwaka huohuo nilianza kutunga nyimbo chache nikiwa najifunza. Wimbo wangu wa kwanza kutunga ulikuwa ni: "KINYWA CHANGU KITASIMULIA". Wimbo huu unapatikana pia kwenye tovuti ya nyimbo za kanisa ya "www.swahilimusicnotes". Mpaka sasa nimejaliwa kutunga nyimbo zaidi ya 200, zinazoimbwa ndani na nje ya Tanzania.
Mwaka 2024 nimetimiza miaka 30 ya uimbaji na pia miaka 20 ya utunzi na kucheza kinanda.
Namshukuru sana Mungu wangu kwa wema wake kwangu, namuomba aendelee kunijalia uzima na baraka ili nimtumikie daima!.
Kwaya ambazo nimewahi kuimba ni pamoja na: