Ingia / Jisajili

Inocent F Shayo

Mfahamu Inocent F Shayo, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki. Kutoka Jimbo la Same Parokia ya Chanjale - St. Stephen

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 89 > Zitazame

Jimbo analofanya utume: Same

Parokia anayofanya utume: Chanjale - St. Stephen

Namba ya simu: +255 755 472 721

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Mwl. Inocent F. Shayo ni mkristo mkatoliki ambaye nimetumika kama mwalimu wa kwaya  kwa takribani miaka saba sasa. Nilianza rasmi kufundisha kwaya  mnao mwaka 2009 ambapo kwaya yangu ya kwanza kuifundisha na kupiga kinanda ilikua ni kwaya TYCS Same sekondari.

Mimi ni mwalimu  wa kwaya, mtunzi wa nyimbo na mpiga kinanda. Namshukuru Mungu kwa utume na huduma hii aliyonipatia,kwa  hakika ni kwa neema tu ndio maana amenipa haya. Tangu nimeanza huduma na utume huu nimefundisha kwaya mbalimbali kama vile Kwaya  ya TYCS Same Sekondari, kwa kuu ya Mt. Yosefu Mfanyakazi - Parokia ya Same jimbo la Same, kwaya ya Mt. Secilia  Parokia ya Hedaru Jimbo la Same, kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia teule ya Chuo kikuu cha Dodoma  UDOM Jimbo la Dodoma, kwaya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi COED parokia ya Chuo kikuu cha Dodoma, Kwaya ya Mt. Secilia Parokia ya Ndugu jimbo la Same na Kwaya ya Mt. Stefano Shule ya Sekondari ya St. Stephen. Pamoja na kufundisha kwaya hizo kama mwalimu, pia nimewahi kufanya kazi tofauti tofauti na kwaya mbalimbali kwa vipindi vifupi vifupi au kwa muda maalumu. Kwa sasa nafundisha kwaya ya Mt. Stefano shule  ya sekondari St. Stephen.

Nimetunga nyimbo mbalimbali takribani 100 mpaka sasa. baadhi ya nyimbo hizo zinapatikana swahili music na baadhi bado sijafanikiwa kuziingiza. Baadhi ya nyimbo zangu zimerekodiwa na kwaya mbalimbali hapa nchini. Utunzi wangu hujikita katika maudhui tofauti tofauti, zipo nyimbo maalumu za liturjia yaani  nyimbo za mwanzo na Katikati lakini zipo ambazo zina mrengo wa kufundisha na kuelimisha jamii.

Nimefanikiwa kutengeneza albamu yangu, yaani nimekusanya nyimbo zangu kadhaa na kuzirekodi na kwaya ya Moyo Mtakatifu wa Yesu UDOM katika albamu ijulikanayo kama Usiifukie Talanta.

Kwa hakika ninafurahi na kujivunia katika huduma na utume huu Mungu alionijalia.  Nimepiga hatua kubwa ukilinganisha na nilipoanzia kwani kazi haikua rahisi sana,  japo bado najifunza na nitaendelea kujifunza kwani kila siku kuna mambo mapya ya kujifunza.Asante sana Mungu kwa kunichagua mimi niliye mdogo.