Ingia / Jisajili

Peter Makolo

Mfahamu Peter Makolo, mtunzi wa nyimbo za Kanisa Katoliki.

Maelezo zaidi

Idadi ya nyimbo SMN: 21 > Zitazame

Namba ya simu: +46 739 635 772

Soma Historia na maelezo yake hapa

Wasiliana na mtunzi kwa email:


Historia / Maelezo

Mzaliwa na mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga, ameanza kuimba 1989 kigango cha Mhunze Parokia ya Ndoleleji.
 
Alianza kujifunza kupiga kinanda mwaka 1993 baadae alianza kujifunza muziki mwaka 1994 chini ya walimu CHANYA (RIP) na DACHA. Baadae aliendelea kujiendeleza kimuziki zaidi Nyegezi Seminari Mwanza, 1997-2000 na baadae Ilboru Arusha 2001-2003. Aliendelea kujiendeleza kimuziki zaidi katika Parokia ya Chuo Kikuu DSM tangu 2004 hadi sasa. Alibahatika kuhudhuria kozi za muziki kwa muhula mmoja chini ya Mwalimu John MGANDU (RIP) chuo Kikuu DSM.
 

Kazi: Mwajiriwa wa Chuo Kikuu DSM, Mkufunzi - Idara ya Uhandisi wa Umeme.

Kwaya anayoimbia: Mt. Augustino - Chuo Kikuu DSM (Sauti zote)

Kwa sasa: Yuko masomoni Sweden