Mtunzi: Moyo Jr
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 3,548 | Umetazamwa mara 8,352
Download Nota Download Midi1. Nani angenijalia uzima kama Mungu ni nani angenijali kama yeye
Nani angenijalia neema kama Mungu ni nani angenipa heshima kama yeye
Daima nitamuimbia nyimbo za kumsifu Mungu
KIITIKIO:
Acheni nimwimbie nimtumikie yeye ni mwema acheni nimsifu Mungu wangu yeye anipenda x2
2. Ni nani angeniinua mimi kama Mungu nani angenipa nguvu kama yeye
Nani angenipatia amani kama Mungu ni nani angenipenda kama yeye
Daima nitamuimbia….
3. Nani angenipatia furaha kama Mungu nani angenikubali kama yeye
Ni nani angenilinda salama kama Mungu nani kweli angeniponya kama yeye
Daima nitamuimbia….
4. Ni mmoja anipiganiaye ndiye Mungu kweli anipenda sana ndiye yeye
Ni ngome yangu na kinga yangu ndiye Mungu yeye ni nguvu yangu ndiye yeye
Daima nitamuimbia….