Mtunzi: Tumshangile Bwana
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Eric Mwaniki
Umepakuliwa mara 148 | Umetazamwa mara 215
Download Nota
Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Amin kweli, nawaambieni mwanitafuta.
Si kwa sababu mlikula ule mkate.
Si kwa sababu mliziona zile Ishara.
Bali sababu mlikula mkashiba *2
Amin, amin, nawaambieni kuna chakula kinachowafaa,
Nacho chakula ndicho kile cha uzima wa milele
2. Msikitendee kazi chakula kinachopita.
Bali, chakula kidumucho milele.
Chakula Musa alichowapa hakiwafai,
Kweli Babangu anawapa kifaacho
3. Kile chakula chenye uzima kweli ni mimi
Ajaye kwangu hataona njaa kamwe.
Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
Hukaa kwangu nami hukaa ndani yake.
4. Hicho chakula chenye uzima kweli ni mimi.
Kilichoshuka toka mbinguni kwa Baba.
Mtu akila chakula hiki hatafariki.
Bali anao ule uzima wa milele.
5. Kile chakula ninachotoa ni mwili wangu,
Kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
Msipokula huu mwili wake mwana Adamu.
Hamna 'zima ndani yenu.
6. Anayekula huu mwili wangu na kuinywa damu
Ana uzima, nami nitamfufua.
Na mwili wangu ndicho chakula kile cha kweli.
Na damu yangu ndicho kinywaji cha kweli
7. Na kama Baba aliye hai 'livyonituma,
Nami ni hai, ndimi hai kwa Babangu.
Na kadhalika, mwenye kunila ana uhai,
Kweli nasema atakuwa hai kwangu,