Ingia / Jisajili

Asante Mungu

Mtunzi: Eric Onsakia
> Mfahamu Zaidi Eric Onsakia
> Tazama Nyimbo nyingine za Eric Onsakia

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Mwaka Mpya | Shukrani

Umepakiwa na: Felix Owino

Umepakuliwa mara 464 | Umetazamwa mara 816

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
ASANTE MUNGU. Asante Mungu wangu kwa mema uliyonijalia x2; Nakushukuru Bwana, Muumba wa vitu vyote, mimi kiumbe chako, nitakusifu milele asante x2 1.Umenilinda vyema, katika maisha ukanijalia afya njema ya mwilini 2.Umenilinda vyema, katika safari ukaniepusha na ajali za njiani 3.Wanipenda hakika, na kunijali tangu utoto wangu wala hukunitupa 4.Mimi ni kitu gani, hata unijali thamani yangu kweli si kitu mbele yako 5.Ee Mungu wangu mimi, ninakupenda fadhili zako kwangu mimi nimeziona 6.Maisha yangu yote, nakuachia ili moyo wangu ushinde upendo wako
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa