Mtunzi: S. D. Masanja
> Tazama Nyimbo nyingine za S. D. Masanja
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Ludovick Michael
Umepakuliwa mara 1,764 | Umetazamwa mara 4,201
Download Nota Download MidiBETHLEHEMU KAZALIWA MTOTO
Bethlehemu amezaliwa, amezaliwa leo mtoto Yesu ( Bethlehemu amezaliwa mtoto, amezaliwa leo mwana wa Mungu) x2
Bethlehemu amezaliwa, amezaliwa leo mtoto Yesu (Waamini njoni tumsujudie, kama vile mamajusi walivyofanya, tutoe na zawadi kwake mwana wa Mungu) x2
1. Twende wote hima tukamwabudu mtoto, twende na zawadi tukamtolee mtoto.
2. Yeye ni masiha aliyeleta wokovu, wokovu kwa watu wenye kumtumaini.
3. Yeye ni mfalme tena mfalme wa ajabu, yeye ni Bwana na ndiye Bwana wa mabwana.