Ingia / Jisajili

Bikira Maria

Mtunzi: Alexander Francis Sitta
> Mfahamu Zaidi Alexander Francis Sitta
> Tazama Nyimbo nyingine za Alexander Francis Sitta

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Alexander Francis Sitta

Umepakuliwa mara 1,468 | Umetazamwa mara 4,908

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

Bikira Maria mama wa Mungu wewe ndiwe mama yake Yesu kristu mkombozi wetuX2. Utuombee mama utuombee mama tuombee kwa mwanao Yesu ili tuhesabiwe miongoni mwa watakatifu wa Mungu X2.

Mabeti

1.Wewe kimbilio la wakosefu,pia ndiwe mwombezi wa wagonjwa,utuombee kwa mwanao utuombee mama.

2.Utulinde mama na yule mwovu,upendo utawale kati yetu,utuombee kwa mwanao tuombee mama.

3.Ndiwe mfariji wa wenye uchungu,na sababu ya furaha yetu,utuombee kwa mwanao tuombee mama

4.Ee mama wa shauri jema,utuombee sisi wakosefu,ave ave ave Maria ave Maria.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa