Mtunzi: Frt. S. Magangila
> Tazama Nyimbo nyingine za Frt. S. Magangila
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Vusile Silonda
Umepakuliwa mara 2,437 | Umetazamwa mara 7,988
Download Nota Download MidiMama Maria Malkia wa Amani utulinde Mama sisi na taifa letu Salamu twakusalimu, uliyejaa neema, Ndiwe Mama yetu na faraja yetu sote uilinde Mama nchi yetu Tanzania tunaleta ombi letu utusikie ee Mama, Bikira Malkia wa Amani. Salaam Malkia mfariji wetu siku zote Mama, Sisi wana wako tunaomba utupe Amani Maria Utukinge na shetani tuepushe na yule mwovu na makucha yake twaomba utulinde Mama Utuombee ee Mama tusimamie ee Mama sisi wakosefu hata saa ya kufa kwetu
1. Wakatoliki wote tuna jukumu la kusema asante kwa Mama Bikira Maria Malkia wa Amani
2. Waamini pamoja tuungane tusali Rozari tumuombe Mama Maria atufikishe mbinguni
3. Katika Parokia zote za jimbo tutembeze sanamu ya Mama Bikira Maria msimamizi wa Jimbo letu
4. Tusali Litania ya Maria ili kumheshimu na kumpongeza Bikira aliyejaa upendo na unyenyekevu
5. Bikira Maria Malkia wa amani tuombee ee Mama kwa mwanao Yesu Kristo ili nasi siku moja tufike mbinguni