Mtunzi: Boniventure John Oisso
> Mfahamu Zaidi Boniventure John Oisso
> Tazama Nyimbo nyingine za Boniventure John Oisso
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: BONIVENTURE OISSO
Umepakuliwa mara 683 | Umetazamwa mara 2,027
Download Nota Download Midi( Bwana amejaa Huruma na Neema ) X2
Maashairi
1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
2. Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,
Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema.
3. Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,
Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
Alimjulisha Mussa njia zake,
Wana wa Israel matendo yake.
4. Bwana amejaa Huruma na Neema,
Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.
Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa waamchao.