Ingia / Jisajili

Bwana Ninakuja Kwako

Mtunzi: Evaristo Mfanyakazi

Makundi Nyimbo: Miito

Umepakiwa na: Joseph Isaya Mwakapila

Umepakuliwa mara 437 | Umetazamwa mara 1,467

Download Nota
Maneno ya wimbo

Kiitikio; Bwana ninakuja kwako mimi mwana wa mjakazi wako; uliyenitwaa kutoka katika kizazi kile dhaifu.

Ninakuomba Bwana wangu nipe neema zako (Bwana), nikatangaze neno lako kwa mataifa x 2

  1. Ee Bwana umenipima ukanijua mimi, ninavyoketi na ninavyosimama mimi, ukaniweka (mimi) panapo nafasi.
  2. Nilipoangushwa chini nao wabaya wangu, hukuniacha mimi mwanao niangamie, ukanishika (mkono) na kuniokoa.
  3. Adui zangu walipotaka niaibike, Bwana hukuwapa nafasi ya kufanya hivyo, ukaharibu (mawazo) yao mabaya.
  4. Hakika Bwana wewe u karibu na wanyonge, huwahifadhi wote waliopondeka moyo, huwafariji (walio) kata tamaa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa