Mtunzi: Sammy Ikua
> Mfahamu Zaidi Sammy Ikua
> Tazama Nyimbo nyingine za Sammy Ikua
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Sammy Ikua
Umepakuliwa mara 1,462 | Umetazamwa mara 3,960
Download NotaBWANA USINIKEMEE
Bwana usinikemee kwa hasira yako, usinirudi kwa ghadhabu yako. X2
Kweli mimi mwenye dhambi nimekosa
Kwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo.
Bwana nisamehe. X2
1. Natamani kuwa nawe, pia kuitwa mwanao, lakini ninazo dhambi, sifai mbele zako.
2. Mimi mwana mpotevu, nimerudi kwako Baba, naomba unisamehe, nipokee kwako Baba.
3. Shida zangu za mwilini, pia shida za rohoni, nazileta kwako Baba, Baba uniondolee.
4. Ni aibu kwangu mimi, mimi kuwa mwenye dhambi, nikikumbuka mwanao, alikufa niokoke.