Mtunzi: J. Mgango
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Joseph Isaya Mwakapila
Umepakuliwa mara 1,823 | Umetazamwa mara 4,218
Download NotaNinapo kula mwili wako Ee Bwana moyoni (Bwana) mwangu hujaa furaha
Ninapokunywa damu yako Ee Bwana moyoni (Bwana) mwangu hujaa furaha
Chakula hiki Bwana kitokacho mbinguni Kinywaji hiki Bwana kitokacho mbinguni kweli ni uzima Bwana nipe siku zote ukae ndani yangu Bwana nami ndani mwako milele na milele x2
1. Nilishe Bwana ninakuomba, Ninyweshe Bwana ninakuomba, Chakula hiki Bwana chenye uzima (uzima) wa milele
2. Bahati gani nimeipata, Kufika hapa altareni, nile Chakula (Bwana) chenye uzima wa milele.
3. Ninatamani niwe na wewe, Nimejongea kwenye karamu, nile Chakula (Bwana) chenye uzima wa milele.
4. Huruma Bwana msaada wako, Ninakuomba kwa moyo wote, nile Chakula (Bwana) chenye uzima wa milele.
5. Ingia Bwana ndani mwangu, Niwe wako siku zote, nipe Chakula (Bwana) chenye uzima wa milele