Ingia / Jisajili

Dunia Yetu

Mtunzi: Augustine Rutakolezibwa
> Mfahamu Zaidi Augustine Rutakolezibwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Augustine Rutakolezibwa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: AUGUSTINE RUTAKOLZIBWA

Umepakuliwa mara 631 | Umetazamwa mara 2,895

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

DUNIA YETU

1. Nikitazama pande zote za dunia uliyoumba,

    naona mabara yote ya dunia na vyote vilivyomo,

     ninajua kwamba ee Mungu wewe umeumba haya yote,

      ili mwanadamu aishi na kukutukuza wewe Mungu

KIITIKIO; Wito, wito umetolewa, tuifanye dunia yetu mahali pema pa kuishi x 2

2. We we ulimuumba  m-tu, kwa sura na m-fano wako,
     si mweupe wala mweusi, wote wanafanana na wewe,
     Leo dunnia yashuhudia, ubaguzi kati ya watu,
     Eti wengine ndio bora, kiliko wale watu wengine...WITO
 
3.Leo vita vinatokea, kati yazo n-chi nan-chi,
   makabila ndugu na wale, walio na dini tofaouti,
   wakubwa nao matajiri,leo wamekosa upendo,
   kwa wale walio wadogo maskini wasiojiweza.....WITO
 
4.Machafuko sasa ni mengi, kwa pande zote za dunia,
   madaraka dini siasa, vimekuwa vyanzo vya ugomvi,
  nani aje kutunusuru, kututoa kwenye majanga,
 kwani ukombozi wa dunia, uko katika Kristu Yesu...WITO
 
5.We we Bwana Mungu Mwenyezi, ulimtuma mwanawako,
    akafia m-salabani, ili watu tupate kuishi,
    Lakini leo twasahau, kazi ya ukombozi wetu,
    tuungane sote pamoja, kwani Yesu ndiye kimbilio....WITO
 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa