Ingia / Jisajili

Ee Bwana Nakuinulia Nafsi Yangu

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Majilio

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 3,675 | Umetazamwa mara 9,141

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

EE BWANA NAKUINULIA NAFSI YANGU

Ee Bwana ee Bwana nakuinulia nafsi yangu ee Mungu wangu, nimekutumaini wewe nisiaibike;
Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda, adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.

1. Naam wakungojao hawataaibika, hawataaibika, hawataaibika hata mmoja, wataaibika wale wote wakuasio, wakuasio Bwana kwa makusudi.

2. Unijulishe njia zako ee Bwana, unifundishe mapito yako uniongoze katika kweli, kweli yako, kwani wewe ni Mungu pia Mwokozi wangu nakutegemea wewe kila siku.

3. Uzikumbuke rehema zako ee Bwana, na ukumbuke  fadhili zako kwa maana zimekuwako toka zamani,usikumbuke dhambi za ujana wangu nikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako.


Maoni - Toa Maoni

jeremia juma Nov 11, 2016
Samahani, mbona nyimbo nazidanloawd haziimbi hata dakika2? Wala hazichukui hata MB hata 3 ivi? au ni kiyonjo2 mnatoa? mbona nakuwa sielewi jamani? TUMSIFU YESU KRISTO.

Toa Maoni yako hapa