Ingia / Jisajili

Ee mungu mwenyezi ninakuja mbele yako

Mtunzi: John Kimaro
> Mfahamu Zaidi John Kimaro
> Tazama Nyimbo nyingine za John Kimaro

Makundi Nyimbo: Kwaresma

Umepakiwa na: John Emanueli

Umepakuliwa mara 247 | Umetazamwa mara 1,038

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
KIITIKIO; Ee mungu mwenyezi ninakuja mbele yako, ninakulilia ( Mimi) nikiomba msaada wako( uwe kiongozi wangu) katika Safari yangu, nakuomba Ee mungu, niongoze Mimi katika Safari yangu. Vikwazo vya dunia( mimi) vinanisonga, matatizo ya dunia(Mimi) yaniandama nakuomba mungu nisaidiex2. MASHAIRI; (1) dunia imenielemea Mimi shetani muovu ananiendesha nakuomba mungu wangu unisaidie. (2) Napiga goti mbele yako mungu ninalia Mimi kwani magonjwa yananielemea nakuomba mungu wangu unisaidie. (3) Safari hii niliyokutumia mimi Ni Safari yenye vikwazo vingi Sana nakuomba mungu wangu unisaidie. (4) misiba mingi imeniandama ninalia Mimi bwana machozi yanafumba macho yangu nakuomba mungu unisaidie. (5) shetani muovu ananiandama ananishawishi nimfwate yeye nakuomba mungu wangu unisaidie. (6) ninakuomba Ewe mungu wangu nitende mema ili nifike huko mbinguni kwako ili nifurahi na watakatifu wote.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa