Ingia / Jisajili

Ee Mungu Twalilia Amani

Mtunzi: Michael Shija
> Mfahamu Zaidi Michael Shija
> Tazama Nyimbo nyingine za Michael Shija

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Michael Shija

Umepakuliwa mara 720 | Umetazamwa mara 2,989

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Oh Ee Mungu ii Ee Mungu twalilia amanix2

Dunia tunayoishi Baba imejaa machafu

Binadamu twauana baba tene bila ya hatia

Oh Baba tazama machozi yetu

Oh tunayolia kuomba amani

MASHAIRI

  1. Tazama baba ndugu zetu walema wa ngozi wanavyouawa
    Amani imetoweka kwao kila siku na mashaka
    Oh Mungu waokoe ndugu zetu,oh Mungu wanahaki ya kuishi.
  1. Tazama Baba hata viumbe ambao bado hawajazaliwa
    Hawana amani wanahofu ya kutolewa tumboni
    Oh Mungu waokoe ndugu zetu, oh Mungu wanahaki ya kuishi
  1. Tazama Baba vikongwe wanauawa kwa yuhuma za uchawi
    Wakati wewe Baba umewajalia maisha marefu
    Oh Mungu waokoe ndugu zetu, oh Mungu wanahaki ya kuishi
  1.  Tazama Baba mataifa mengi duniani yanavyopigana
    na kuua viumbe wako uliowaweka duniani
    Oh Mungu waokoe ndugu zetu, oh Mungu wanahaki ya kuishi.

HITIMISHO.

Nyoosha mkono wako Baba waangamize wote, wanaovuruga amani duniani,

(Baba kamaulivyo yaangamiza majeshi ya Farao) x2

Wafedheheshe hao, Baba twaami utatenda

Wasiue albino, Baba twaamini utatenda

Wasiue vikongwe, Baba twaamini utatenda

Wasizitoe mimba, Baba twaamini utatenda

Waache mapigano, Baba twaamini utatenda

Tuishi kwa amani, Baba twaamini utatenda


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa