Ingia / Jisajili

Giza Nene Limetanda (Niongoze Mama Maria)

Mtunzi: Victor Murishiwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Victor Murishiwa

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: James Lunalo Khalwale

Umepakuliwa mara 1,404 | Umetazamwa mara 3,959

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NIONGOZE MARIA

Niongoze mama Maria, nionyeshe njia ya kweli (ya kweli) ya kunifikisha mbinguni kwa mwanao Yesu x2.

  1. Giza nene limetanda, (limetanda mbele yangu x2); limenifunika macho nitakwenda wapi mimi na unyonge wangu huu.
  2. Mama Bikira Maria msaada wa wagonjwa, kimbilio la wanyonge. Nakukimbilia Mama niombee kwa Mwanao aniponye roho yangu.
  3. Kwa rozari yako Mama ninapata tumaini la uzima wa milele. Ewe Mama wa huruma unifute chozi langu, hofu zote zinitoke.
  4. Ewe ua la waridi nifunike bawa zako, nilipate joto lako, katika safari yangu unilinde na hatari zinazo ninyemelea.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa