Mtunzi: Ochieng' Odongo
> Tazama Nyimbo nyingine za Ochieng' Odongo
Makundi Nyimbo: Mwanzo
Umepakiwa na: Silvanos Wamalwa
Umepakuliwa mara 2,451 | Umetazamwa mara 5,702
Download Nota Download Midi1. Mbona mnachezacheza na kushangilia - sisi tunafurahia maajabu ya Mungu.
Mbona mnaimbaimba kwa sauti nzuri - sifa zake zi vinywani mwetu siku kwa siku.
Haya njooni, mkaonje muone ya kwamba Bwana yu mwema (sana)
Haya njooni, mkaonje muone ya kwamba Bwana yu mwema
2. Aliumba mbingu yote akaumba na nchi - vitu vionekanavyo na visivyoonekana.
Yeye afanyaye jua lisiwake usiku - wala mwezi nazo nyota zisiwake mchana.
3. Asubuhi na mapema ndege humuimbia - wanamshukuru Mungu kwa maisha mazuri.
Samaki wa baharini wanaruka kwa shangwe - wote wanafurahia nehema yake Mungu.
4. Tumaini letu sisi ni kwa Mungu mwenyezi - kwa maana yeye ndiye aliye na uwezo.
Tazameni kwake juu na mtatiwa nuru - wala nyuso zenu kamwe hazitaona haya.
5. Basi mtukuze Bwana wetu pamoja name - tuliadhimishe jina lake sote pamoja.
Utawala na uweza wote ni wake yeye - jina lake litukuzwe daima na milele