Mtunzi: Benedict Werema
> Tazama Nyimbo nyingine za Benedict Werema
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Benedict Weise
Umepakuliwa mara 14 | Umetazamwa mara 2
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya Pasaka
Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana; tuishangilie na kuifurahia*2
1. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana wema wake ni wa milele. Israeli na aseme sasa: / wema wake ni wa milele.
2. Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa, mkono wa kuume wa Bwana umetenda makuu. Sitakufa, bali nitaishi / nami nitayasimulia matendo ya Bwana.
3. Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Jambo hili alilifanya Bwana; / nalo ni la ajabu machoni petu.