Ingia / Jisajili

Hodi Hodi Ninabisha (Ngo! Ngo! Ngo!)

Mtunzi: Elijah M Kilonzi
> Mfahamu Zaidi Elijah M Kilonzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Elijah M Kilonzi

Makundi Nyimbo: Mwanzo

Umepakiwa na: ELIJAH Mulei

Umepakuliwa mara 439 | Umetazamwa mara 1,138

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Mwanzo Dominika ya 33 Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Hodi hodi ninabisha, ninabisha nyumbani mwako;

Bwana Mungu unifungulie niingie nyumbani mwako;

(ninabisha hodi, ngo! ngo! ngo! unifungulie; njoni wote tumwabudu Bwana)x2

1. Wakusanyikao kwa ajili yangu - Bwana asema yu kati yao

Kwa kukusanyika leo natujue - Bwana Mungu yu kati yetu

2. Umenitendea mema mengi kweli - wema wako hauna mwisho

Kwa mema ambayo umenitendea - naja Bwana nikushukuru

3. Njoni kwangu wale mmelemewa - na mzigo niwapumzishe

mzigo wa dhambi kanichosha mimi - naja Bwana nipumzishe

4. Naileta sala yangu kwako Bwana - nakusihi isikilize

Na sadaka yangu Ee Bwana naleta - ibariki ifae kwako


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa