Mtunzi: Venance Fidelis Nkolabigawa
> Mfahamu Zaidi Venance Fidelis Nkolabigawa
> Tazama Nyimbo nyingine za Venance Fidelis Nkolabigawa
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Venance Nkolabigawa
Umepakuliwa mara 418 | Umetazamwa mara 1,280
Download Nota Download MidiHONGERA MOSES NA HILDA
Kiitikio
Hongera wapendwa wetu hongera sana ee Mo-ses na Hilda Eeeee, Leo mmefunga ndoa yenu hongera sana ee
Mtunze viapo vyenu mlivyoapa ee, Mungu Baba awabarikiiiiiii, muishi maisha ya furaha na baraka tele
Mashairi
1. Mungu Baba awalinde muishi kwa upendo, muishi kwa amani siku zote za maisha yenu.
Kuishi kwenu wawili ni kuvumiliana na kusameheana kwa moyo wa mapendo, (Moses) na Hilda ee Iweni
watoto wa Mungu mtayashinda yote.
2. Mpendane siku zote ka-tika taabu na katika ra-ha shetani asiwavu-ruge.
Msifungue Milango kwa hodi za shetani, atawavuruga vichwa atawasambaratisha, (Moses) na Hilda ee.........
3. Mmeamua wenyewe kuweka maagano, muyatunze ve-ma msije mkayavu--nja.
Mpendana wenyewe wala sio kwa shuruti, mlitunze pendo lenu hata mkae wazee, (Moses) na Hilda ee.........