Ingia / Jisajili

Hostia Takatifu

Mtunzi: S. N. Ndeketera

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Gervas Kombo

Umepakuliwa mara 3,219 | Umetazamwa mara 7,127

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Hostia ta (Jioni Al)

Hostia ta (Jioni Al)

Hostia takatifu ni wili wa Yesu

Hostia takatifu usiku wa teso

Ashika Yesu mkate mikononi kuleni nyote huu ni mwili wangu

1.       Mwili na damu ya Bwana chakula cha uzima, Ee kiumbe duni sana wamla Bwana Yesu

2.       Ee Yesu ninasadiki katika mkate huu Nakuona kwa imani mwili na damuyo

3.       Ekaristi ni fumbo la mwili wa Yesu Ee kiumbe duni sana wamla Bwana Yesu


Maoni - Toa Maoni

Innocent B Apr 09, 2020
Huu wimbo niliusikia kwa mara ya kwanza mwaka 1992 nikiwa kijijini nilikozaliwa baada ya kumaliza kulitumikia jeshi la kujenga taifa kwa compulsory baada ya kumaliza kidato cha sita na kabla ya kujiunga chuo kikuu. Niliupenda sana kwa kuwa sauti na mashairi na kiitikio ni nzuri mithili ya sauti za malaika. Sikujua wapi pa kuupata. Nilizungukia sehemu mbalimbali ikiwemo Radio Tanzania na makanisa mbalimbali kupata cassette yake. Kwa muda wa miaka 10 niliutafuta bila kukata tamaa. Mwaka 2003 nilibahatika kwenda Arusha kwa wiki mbili. Niliulizia wimbo huo ambao sikujua mtunzi bali nilikuwa ninaimba sehemu ya wimbo huo kuutafuta. Nikaambiwa umeimbwa na KVT Arusha lakini sikuupata wakati huo kwa vile mtunza funguo wa sehemu ya kuweka cassette za kwaya alikuwa amesafiri. Mwaka uliofuata 2004 nilienda tena kikazi Arusha na ndipo nilipobahatika kupata cassette yenye wimbo huo. Niliupata baada ya kutafuta kwa miaka 10!

George Fumbuka Aug 04, 2017
Classic! Can you upload it in You Tube or where can I find it. Who is the Author? What is he? Many thanks on advance.

Camilius Jun 19, 2017
Hongera kwa utunzi mzuri Mungu akuzidishie afya ya mwili na roho umtukuze kupitia utunzi was nyimbo nataman siku walau hata siku moja na mm nijue utunzi wowote wa kumtukuza Mungu

Edward Ferdinand Lukwimbi Apr 02, 2017
Huu wimbo wa Hostia Takatifu uliotungwa na Ndekitera Mbona sauti ya nne hawajawekewa maneno yao wanayoimba maana inachanganya.

Toa Maoni yako hapa