Ingia / Jisajili

Janga La Ukimwi

Mtunzi: Davis Milenguko
> Tazama Nyimbo nyingine za Davis Milenguko

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 685 | Umetazamwa mara 2,807

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Siku miezi miaka yapita,
Ndugu tunakwisha (kweli) ni mateso,
Tumevamiwa nalo janga la UKIMWI
Ee Mungu Baba Tusaidie.
 
2.Nini cha kufanya wote twajua,
 Jama tuchukue (kweli) tahadhari,
 Uasherati ngono uzembe mitaani,
 Tutateketea wote kabisa.
 
3.Ndugu tega sikio ufahamu,
 Na dalili zake (kweli) zitambue,
 Homa za mara kwa mara zitatokea,
 Pia uzito wako kupungua.
 
4.Ona wagonjwa wanavyoteseka,
 Wataalamu wetu (kweli) wameshindwa,
 Kupata tiba ya hili gonjwa UKIMWI,
 Ndugu wote tubadili mtazamo.
 
5.Tuwakumbuke na waathirika,
 Tuwapende wote (kweli) tuwatunze,
 Hawakupenda wanyanyaswe na UKIMWI,
 Ndugu leo kwangu na kesho kwako.
 
6.Waziri nanyi viongozi wetu,
 Mtufundisheni (kweli) tutambue,
 Hata tupange maamuzi ya Busara,
 Tusubiri ili tunusurike.
 
7.Dunia yote inasikitika,
 Ulimwengu mzima (kweli) unalia,
 Vizazi vinaangamia na UKIMWI,
 Mungu tuokoe na janga hili.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa