Ingia / Jisajili

Jioni Alhamisi

Mtunzi: Dionizi Kipanya
> Tazama Nyimbo nyingine za Dionizi Kipanya

Makundi Nyimbo: Juma Kuu

Umepakiwa na: Emmanuel Shimbala

Umepakuliwa mara 605 | Umetazamwa mara 1,725

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Jioni Alhamisi usiku wa teso, ashika Yesu mkate katika mikono.

Ashika kikombe cha divai, asema twaeni mle mkanywe nyote.

  1. Je! mwafahamu niliyotenda, huu ndio mwili wangu, kuleni mpate uzima, hiki ni chakula chenu,kuleni mkinikumbuka.
  2. Anayeniamini mimi, na kushika nisemayo,atakuwa ndani yangu mimi, na mi nitakuwa naye, hili ndilo pendo la baba.
  3. Hiki ndicho chakula cha mbingu, si kama mana ya jangwani, walizokula baba zenu, nao nao wakafa, chakula hiki ni uzima.
  4. Si kwa shibe ya tumbo na mwili,wala si kwa utamu, bali kwa uzima wa Roho, na ladha yenye uchachu,ishara ya teso langu kuu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa